Pata taarifa kuu
LIBYA-SIASA-UFARANSA

Viongozi wa Libya kukutana Ufaransa kujadili hali ya kisiasa

Wawakilishi kutoka pande zinazokinzana nchini Libya watakutana jijini Paris nchini Ufaransa siku ya Jumanne wiki ijayo kujadili mustakabali wa kisiasa nchini mwao.

Ulinzi katika mojawapo ya majengo ya serikali jijini Tripoli
Ulinzi katika mojawapo ya majengo ya serikali jijini Tripoli REUTERS/Omar Ibrahim
Matangazo ya kibiashara

Lengo la mkutano huo, ni kujadili namna ya kufanikisha Uchaguzi Mkuu utakaowaunganisha raia wa taifa hilo.

Mazungumzo haya yanaungwa mkono na Umoja wa Mataifa na mataifa ya Magharibi, ikiwemo Ufaransa ambayo rais Emmanuel Macron ndiye atakayekuwa mwenyeji.

Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa, Ghassan Salame kwa muda mrefu sasa amekuwa  akijaribu kushawishi pande zote mbili kuweka kando tofauti zao na kurejesha hali ya kidemokrasia nchini humo.

Libya imeendelea kukosa amani, huku wanajeshi wa serikali wakiendelea kupambana na makundi ya waasi tangu kuuawa kwa kiongozi wa nchi hiyo Muammar Gaddafi mwaka 2011.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.