Pata taarifa kuu
DRC-EBOLA-WHO-KANISA KATOLIKI

Kanisa Katoliki nchini DRC lahofia maambukizi ya Ebola

Kanisa Katoliki nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, linasema lina wasiwasi kuhusu kuendelea kuripotiwa kwa maambukizi mapya ya virusi hatari vya Ebola Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo.

Raia wa DRC wakipewa chanjo ya kuzuia ugonjwa hatari wa Ebola
Raia wa DRC wakipewa chanjo ya kuzuia ugonjwa hatari wa Ebola REUTERS / Kenny Katombe
Matangazo ya kibiashara

Hadi sasa watu 25 wamepoteza maisha na 54 kuambukizwa, huku wengine 1,139 wakiChunguzwa kwa karibu baada ya kukaribiana na watu waliambukizwa.

Kauli hii imetolewa na Askofu wa Kanisa hilo Fridolin Ambongo ambaye ametembelea mji wa Mbandaka na Bikoro maeneo ambayo yameathiriwa na ugonjwa huo.

Askofu Ambongo amesema, hofu imetenda kote katika maeneo yaliyoathiriwa na Kanisa Katoliki, limesitisha kwa muda mikutano ya hadhara ikiwepo, ubatizo na ibada ya kuwasimika makasisi iliyokuwa imepangwa kufanyika tarehe 3 mwezi ujao katika mji wa Mbandaka, imeahirishwa.

Kanisa hilo, limeungana na maafisa wa afya kutoa wito kwa wakaazi wa Kaskazini Magharibi mwa nchi hiyo, kuacha kusaliamiana au hata kugusana na kunawa mikono yao kwa sabuni na maji safi, ili kuepuka kuambukizwa ugonjwa huo.

Shirika la afya duniani WHO, nalo limeedelea kutoa chanjo katika njia mojawapo ya kupambana na ugonjwa huu hatari.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.