Pata taarifa kuu
MISRI-HRW-USALAMA

Jeshi la Misri lashtumiwa kuharibu mali za wakazi wa Sinai

Shirika la Kimataifa la Haki za Binadamu,Human Rights Watch, limeshtumu jeshi la Misri kuendelea na operesheni yake ya kubomoa majengo katika jimbo la Sinai, kama sehemu ya kampeni ya kijeshi dhidi ya kundi la waasi lenye uhusiano na kundi la Islamic State (IS).

Vikosi vya kijeshi vay Misri kaskazini mwa Sinai.
Vikosi vya kijeshi vay Misri kaskazini mwa Sinai. REUTERS/Mohamed Abd El Ghany
Matangazo ya kibiashara

Operesheni hii ni kubwa tangu jeshi la Misri lilianza rasmi mpango wake wa kufukuza wakazi mwaka 2014 ili kuunda na ukanda wa Gaza.

"Operesheni hiyo ambayo kwa sehemu kubwa ni kinyume cha sheria, inaendeshwa hadi mbali ya maeneo yaliyotengwa na serikali kwa ajili ya usalama," Human Rights Watch imesema katika taarifa yake.

Kwa mujibu wa Human Rights Watch, operesheni hiyo inahusisha mamia ya hekta za ardhi ya kilimo na majengo 3,000 angalau ya makazi na biashara, pamoja na majengo 600 yaliyoharibiwa Januari.

"Jeshi la Misri linadai kuwa linawalinda watu dhidi ya wapiganaji wa kundi hilo, lakini ni ajabu kufikiri kuwa uharibifu wa makazi na kuhamishwa kwa raia kutahakikisha usalama wao," amesema mkurugenzi wa Human Rights Watch Mashariki ya Kati na Afrika ya Kaskazini, Sarah Leah Whitson, akinukuliwa katika taarifa hiyo.

Jeshi la Misri halijazungumza chochote wakati huu kwa madai ya Human Rights Watch, lakini katika siku za nyuma lilikanusha ripoti za Human Rights Watch kuhusu Sinai, zikinukuu, kwa mujibu wa jeshi, vyanzo visvyoaminika.

Vikosi vya usalama vya Misri vilizinduliwa mwezi Februari operesheni kubwa ya kupambana dhidi ya wanajihadi ambao wanaendesha kwa miaka kadhaa mashambulizi ambayo yamewaua mamia ya askari, polisi na raia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.