Pata taarifa kuu
DRC-EBOLA-WHO

Ebola nchini DRC haijafikia kutangazwa hali ya tahadhari

Mlipuko wa ugonjwa wa Ebola nchini jamuhuri ya demokrasia ya congo haujafikia kiwango cha kutangazwa hali ya dharura kimataifa,limesema shirika la afya duniani WHO.

Baadhi ya madaktari wasiokuwa na mipaka wakiwa nchini DRC
Baadhi ya madaktari wasiokuwa na mipaka wakiwa nchini DRC REUTERS/Tommy Trenchard
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa yake WHO baada ya kukutana na mamlaka ya dharura ya afya imefahamisha kuwa hali ya mlipuko huo haijakidhi vigezo vya kutangazwa hali ya dharura nchini DRC.

Aidha Taarifa hiyo iliongeza kuwa serikali ya Kidemokrasia ya Congo, WHO na washirika wamekuwa na mwitiko wa haraka na wa kina kufuatia hali hiyo.

Tayari shirika la kimataifa la msalaba mwekundu limesema linahamasisha zaidi ya watu mia mbili kujitolea kupambana na ugonjwa huo.

Serikali ya Kinshasa ilitangaza kuzuka kwa virusi vya ebola katika jimbo la kaskazini magharibi Equateur mnamo Mei 8.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.