Pata taarifa kuu
NIGERIA-MAREKANI-USHIRIKIANO

Rais wa Nigeria kuzuru Marekani

Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari anatarajia kuzuru Marekani Jumatatu hii. Hii ni ziara rasmi ya kwanza kwa rais wa nchi ya Afrika tangu Rais wa Marekani Donald Trump kuchukua madaraka nchini Marekani.

Muhammadu Buhari, Septemba 19, 2017 kwenye kikao cvha Umoja wa Mataifa huko New York.
Muhammadu Buhari, Septemba 19, 2017 kwenye kikao cvha Umoja wa Mataifa huko New York. REUTERS/Shannon Stapleton/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Ziara ya Muhammadu Buhari inakuja baada ya ile ya rais wa Ufaransa, Emmanuel Macron na Kansela wa Ujerumani Angela Merkel nchini Marekani. Mkutano kati ya Rais Buhari na mwenyeji wake Donald Trump utazingatia masuala ya usalama na uchumi.

Mwaliko huo ulitolewa mnamo mwezi Januari 2017. Baada ya Donald Trump kukabidhiwa madaraka ya uongozi wa nchi alimpigia simu mwenzake wa Nigeria, Muhammadu Buhari, na kumuomba azuru Marekani.

Ziara hii ya Buhari inakuja miezi kadhaa baada ya Rais Donald Trump kukashifu mataifa ya Afrika.

Kwa kawaida, ofisi ya rais nchini Nigeria haikuweza kutoa taarifa hii, kwani ilikua ilisalia kama siri kubwa kwa taifa hilo. Kwa mujibu wa ikulu ya White House, mazungumzo kati ya wawili hao yatajikita kuhusu vita dhidi ya ugaidi, usalama na uchumi.

Muhammadu Buhari atakuwa kiongozi wa kwanza wa taifa kutoka bara la Afrika kulakiwa na Rais wa Marekani Donald Trump katika ikulu ya White House atakapokutana na kiongozi huyo kwa mashauriano rasmi mjini Washington.

Marais wengine wa Afrika waliwahi kukutana na Bw Trump akiwa rais, ni Paul Kagame wa Rwanda na Uhuru Kenyatta wa Kenya na Rais wa Uganda Yoweri Museveni, lakini nje ya Marekani.

Ziara ya Rais Muhammadu Buhari inakuja ikiwa zimesalia siku chache kabla ya uchaguzi wa urais nchini Nigeria.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.