Pata taarifa kuu
DRC-CENI-SIASA

CENI yaendelea na kampeni kuhusu mashine zitakazotumiwa katika uchaguzi DRC

Tume huru ya uchaguzi nchini DRCongo CENI, inaendelea na kampeni yake ya kuhamasisha raia kuhusu mashine zitazotumiwa katika kupiga kura wakati wa uchaguzi wa Desemba 23, 2018, ambazo zimeendelea kulalamikiwa na baadhi ya wanasiasa wa upinzani.

Afisa wa CENI, Kinshasa. Ceni imeendelea kulaumiwa na upinzani DRC.
Afisa wa CENI, Kinshasa. Ceni imeendelea kulaumiwa na upinzani DRC. AFP PHOTO/ GWENN DUBOURTHOUMIEU
Matangazo ya kibiashara

Siku ya Alhamisi wiki hii, tume hiyo iliwakutanisha wakuu wa idara mbalimbali za serekali yakiwemo mashirika ya kiraia na waandishi wa habari katika tarafa ya Uvira mashariki mwa nchi hiyo ili kuwapa ufafanuzi zaidi wa namna ya kupiga kura kwa kutumia machine hizo.

Hata hivyo upinzani nchini DRC unapinga vikali matumizi ya mashini hiyo ukibaini kwamba ni mbinu za kutaka kuipa kura.

Upinzani ulitishia kutoshiriki uchaguzi iwapo mashine hizo zitatumiwa katika uchaguzi wa urais ujao uliopangwa kufanyika Desemba 23.

Tume ya uchaguzi (CENI) ilionya upinzani na kusema uchaguzi utafanyika hata kama upinzani utakua umesusia.

Hali ya kisiasa nchini DRC imeendelea kusuasua kwa miaka kadhaa, huku upinzani ukiomba Rais Joseph Kabila asiwanii katika uchaguzi huo, jambo ambalo limefutiliwa mbali na chama tawala PPRD na washirika wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.