Pata taarifa kuu
DRC-KATUMBI-HAKI

Kesi ya Moise Katumbi kusikilizwa Juni 26 au 27 DRC

Kesi inayo mkabili mpinzani wa serikali ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo alie uhamishoni Moise Katumbi ambae alitangaza kuwa atawania nafasi ya urais nchini humo Moise Katumbi, itasikilizwa Juni 26 au 27 na mahakama kuu nchini humo, kulingana na wakili wake.

Mawanasiasa wa upinzani nchini DRC alie uhamishoni Moise Katumbi Chapwe, wakati wa uzinduzi wa chama chake cha kisiasa "Ressemblement pour le changement", Machi 12, 2018, Johannesburg.
Mawanasiasa wa upinzani nchini DRC alie uhamishoni Moise Katumbi Chapwe, wakati wa uzinduzi wa chama chake cha kisiasa "Ressemblement pour le changement", Machi 12, 2018, Johannesburg. MUJAHID SAFODIEN / AFP
Matangazo ya kibiashara

Wakili Joseph Mukendi amesema amepokea taarifa hiyo dhidi ya kesi inayomkabili mteja wake kuhusu tuhuma za kuajiri askari mamluki, ambapo uamuzi huo umetolewa na hakuna kukata rufaa baada ya kukwepesha kesi hiyo kutoka Mahakama ya Amani hadi Makama Kuu ya sheria.

Katika hatuwa nyingine, mazungumzo ya chini kwa chini yanaendelea baina ya serikali ya kinshasa na familia ya Marehemu Etienne Tshisekedi wa Mulumba aliefariki mjini Brussels, nchini Ubelgiji sasa ni zaidi ya mwaka kuhusu kusafirisha muili wa kiongozi huyo wa kihistoria wa upinzani nchini DRCongo kwa ajili ya mazishi.

Akizungumza na RFI, Felix Tshisekedi, mwana wa Etienne Tshisekedi, amesema yeye alijiondoa katika mazungumzo hayo kutokana na dharau ya serikali ya DRCongo.

Juma lililopita Felix Tshisekedi aliteuliwa kumrithi baba yake katika uongozi wa chama cha UDPS, hatua ambayo ilipingwa na baadhi ya wafuasi wa chama ambao walifikisha kesi mahakamani kupinga hatua hiyo, kutokana na Waziri Mkuu wa sasa nchini DRCongo Bruno Tshibala kuteuliwa mapema kuchukuwa uongozi wa chama. Hali ambayo iliodhihirisha mpasuko zaidi katika chama hicho kongwe cha upinzani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.