Pata taarifa kuu
SOMALIA-AL SHABAB-USALAMA

Al Shabab yafanya mashambulizi dhidi ya Amisom

Kundi la Al Shabab nchini Somalia limetekeleza mfululizo wa mashambulizi dhidi ya askari wa kikosi cha Umoja wa Afrika (Amisom) na jeshi la Somalia katika mkoa wa Shabelle, kusini mwa Mogadishu.

Askari wa kikosi cha Amisom kutoka Uganda katika mkoa wa Somalia wa Shabelle mnamo mwaka 2014.
Askari wa kikosi cha Amisom kutoka Uganda katika mkoa wa Somalia wa Shabelle mnamo mwaka 2014. AMISOM/TOBIN JONES
Matangazo ya kibiashara

Kundi hilo linasema kuwa lilitekeleza mashambulizi kadhaa dhidi ya kambi za kikosi hicho kinachosimamia amani na usalama nchini Somalia. Kundi la Al Shabab linasema liliwaua askari 59 wa Amisom, wengi wao ni kutoka Uganda, na lilipoteza wapiganaji wake 14 katika vita hivyo. Jeshi la Uganda linasema, kwa upande wake, kuwa wamepoteza askari wanne na wamefaulu kuua magaidi 22.

Kambi kadhaa za Amisom katika moka wa Shabelle zilishambuliwa kwa makombora. Hata hivyo, shambulio la Jumapili, Aprili 1, dhidi ya kambi ya Bulomarer, kilomita 130 kusini magharibi mwa Mogadishu, liligharimu maisha ya askari kadhaa wa Amisom, kwa mujibu wa mashahidi.

Kwa mujibu wa afisa wa jeshi la Somalia, Farah Osman, ambaye alinukuliwa na shirika la habari la Reuters, saa 9:00 asubuhi magari mawili yaliyokua yametegwa mabomu yalianza kulipuka dhidi ya magari ya tume ya Umoja wa Afrika na yale ya jeshi la Somalia. Wakati huo huo wapiganaji wa Al Shabab walifyatua risasi, kabla ya kuendesha shambulio dhidi ya kambi moja.

"Ilikuwa ni vita vikali," amesema afisa huyo jeshi la Somalia.

Anasema wapiganaji wa Al Shabab walifaulu kuingia katika kambi hiyo na kurushiana risasi na askari wa kikosi cha Umoja wa Afrika. Wakati huo huo, bomu lilirushwa dhidi ya msafara wa askari wa Ugandaambao walikua wakitokea katika kijiji cha Golweyn.

Kwa mujibu wa Meja Nur Ali, shambulio hilo dhidi ya kambi ya Bulomarer inaweza kuwa ni ulipizaji kisasi. Siku ya Jumamosi jioni, Amisom na jeshi la Somalia waliendesha operesheni katika maeneo ya vijijini ya mkoa huo.

Shabelle ni mojawapo ya ngome za Al Shabab. Licha ya askari 22,000 na ukaribu wa eneo hilo na Mogadishu, Amisom bado haijafaulu kuondoa kundi hilo la kigaidi katika mkoa huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.