Pata taarifa kuu
TANZANIA-UFARANSA -ELIMU

Ufaransa kuisadia Tanzania kufundisha lugha ya Kifaransa

Serikali ya Ufaransa kuisaidia Tanzania katoa mafunzo kwa walimu wa somo la kifaransa nchini humo ili kuanza kufundishwa kuanzia shule za msingi mpaka elimu ya juu.

Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Frederic Clavier wakati wakifungua majadiliano ya namna ya kuboresha mahuano ya elimu katika vyuo vikuu”
Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Frederic Clavier wakati wakifungua majadiliano ya namna ya kuboresha mahuano ya elimu katika vyuo vikuu” Embasy of France in Tanzania
Matangazo ya kibiashara

Akizungumza wakati akifungua majadiliano ya namna ya kuboresha mahusiano katika sekta ya elimu baina ya nchi hizo mbili jijini Dar es salaam Balozi wa Ufaransa nchini Tanzania Frederic Clavier amesema lengo ni kukuza lugha ya kifaransa nchini humo.

“Tutafanya kila jitihada kuendeleza uhusiano kati ya Ufaransa na vyuo vikuu vua Tanzania,kwa hiyo ni jukumu la wataalam kupendekeza maeneo muhimu katika fani zilizopo “ alisema Clavier

Serikali ya Tanzania imeshindwa kuanza kufundisha lugha ya Kifaransa katika shule za msingi kutokana na ukosefu wa walimu licha ya mtaala kuwepo, Naibu waziri wa Elimu Sayansi na Teknolojia nchini humo William Tate Ole Nasha amesema hali hiyo imetokana na ukosefu wa walimu wa lugha ya kifaransa.

“Sera ipo na mtaala upo isipokuwa ni suala la kusisitiza na kuona namna ambavyo somo la kifaransa litaanza kufundishwa mashuleni kuanzia shule za msingi “ alisema Ole Nasha

Mbali na mpango huo pia serikali ya Ufaransa itasaidia kuwawezesha wanafunzi kujiunga na elimu ya juu nchini Ufaransa katika vyuo vinavyofundisha kwa lugha ya kiingereza katika fani mbalimbali ikiwa ni pamoja na fani za Sayansi.

Wakizungumzia hali ivyo katika vyuo vikuu nchini humo Mkuu wa Idara ya Lugha za Kigeni na Fasihi chuo kikuu cha Dodoma Dakta John Misana Biseko pamoja na Naibu Makamu Kansela wa chuo kikuu cha Dar es salaam Profesa Cuthbert Kimambo walisema mpango huo utatoa fursa kwa wanafunzi wa lugha ya kifaransa kuondokana na kujifunza kwa nadharia pekee.

Mjadilino hayo ya siku mbili yanahusisha vioongozi wa vyuo vikuu nchini Tanzania pamoja na wadau mbalimbali wa lugha na Viongozi wa taasisi inayohusika na ufadhili wa wanafunzi wa elimu ya juu nchini ufaransa.

 

 

 

 

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.