Pata taarifa kuu
ZIMBABWE-MUGABE-MNANGAGWA

Mnangagwa : Mugabe anaweza kusema anachotaka, Zimbabwe imesonga mbele

Rais wa Zimbabwe Emmerson Mnangagwa amesema nchi hiyo imeshapiga hatua baada ya kumwondoa madarakani kiongozi wa zamani Robert Mugabe.

Rais wa Zimbabwe,  Emmerson Mnangagwa
Rais wa Zimbabwe, Emmerson Mnangagwa REUTERS/Denis Balibouse
Matangazo ya kibiashara

Kauli hii imemjibu Mugabe ambaye kwa mara ya kwanza alijitokeza na kusema hatua ya kumwondoa madarakani ilikuwa ni kumpindua kijeshi.

Mugabe alisema alishangazwa sana na hatua ya Mnangagwa ambaye alimsadia kumwingiza kwenye ulingo wa kisiasa, ambaye sasa amembadilikia.

Hata hivyo, Mnangagwa amesema rais Mugabe ana haki ya kusema anachotaka kama raia yeyote wa kawaida.

“Taifa letu limeshapiga hatua. Lengo letu sasa ni kuandaa Uchaguzi Mkuu mwaka 2018,” alisema Mnangagwa.

Uchaguzi utafanyika mwezi Agosti mwaka huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.