Pata taarifa kuu
SOMALIA-SURUA

Watoto zaidi ya Milioni 4 kupewa chanjo dhidi ya surua nchini Somalia

Somalia imezindua kampeni ya nchi nzima ya kuwapa chanjo Mamilioni ya watoto ili kuepuka ugonjwa wa surua.

Kampeni ya chanjo ya suria nchini Somalia
Kampeni ya chanjo ya suria nchini Somalia WHO
Matangazo ya kibiashara

Shirika la afya duniani WHO inasema watoto zaidi ya Milioni 4.7 kati ya umri wa miezi sita na miaka 10, wamelengwa kupata chanjo hiyo.

Watoto wengine Milioni 1.1 wanalengwa kupata chanjo hiyo katika eneo la Somaliland.

Tayari jimbo la Puntland limeshamaliza kutoa chanjo hiyo iliyotolewa mwezi Januari na watoto 933,000 kupewa chanjo hiyo.

Hatua hii ya WHO imekuja baada ya watoto 2,800 kukumbwa na suria katika majimbo ya Bay, Banadir na Mudug.

Idadi hii imeshuka ikilinganishwa na maambuzi ya 23,000 mwaka 2017 hasa dhidi ya watoto chini ya miaka 10 lakini ikafanikiwa kuwapa chanjo watoto zaidi ya 600,000.

Chanjo hiyo itatolewa katika vituo vyote vya afya nchini humo.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.