Pata taarifa kuu
MAREKANI-AFRIKA-ZIARA

Tillerson kuendelea na ziara yake Afrika baada ya kupata nafuu

Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson anatarajiwa kuendelea na ziara yake nchini Kenya siku ya Jumapili, baada ya kuisitisha siku ya Jumamosi baada ya kuripotiwa kuwa alikuwa anajiskia vibaya kiafya.

Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani  Rex Tillerson akiwasili jijini Djibouti Machi 9 2018, moja ya ziara yake barani Afrika
Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Rex Tillerson akiwasili jijini Djibouti Machi 9 2018, moja ya ziara yake barani Afrika Reuters/路透社
Matangazo ya kibiashara

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya nje Steve Goldstein aliwaambia wanahabari kuwa Tillerson mwenye umri wa miaka 65, alikuwa hajiskii vizuri baada ya kazi nyingi nyumbani hasa kuhusu suala la mkutano kukutana kwa kiongozi wa Korea Kaskazini na rais Donald Trump na hivyo alistahili kupumzika.

Mbali na Kenya, Tillerson amezuru Djibouti na Ethiopia na anatarajiwa kumalizia ziara yake wiki ijayo nchini Chad na Nigeria.

Hii ndio ziara ya kwanza ya kiongozi wa juu wa Marekani barani Afrika baada ya kuingia madarakani kwa rais Donald Trump mwaka 2017.

Lengo la ziara hii ni kwa Marekani kuendeleza ushirikiano wa karibu kati yake na mataifa ya Afrika kuhusu masuala ya biashara, usalama miongoni mwa masuala mengine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.