Pata taarifa kuu
DRC-MADINI-KABILA

Rais Kabila kukutana na wawekezaji kwenye sekta ya madini

Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo anakutana na wamiliki wa kampuni mbalimbali za uchimbaji madini kujadili sheria mpya kuhusu sekta ya madini.

Rais wa DRC Joseph Kabila
Rais wa DRC Joseph Kabila REUTERS/Kenny Katombe
Matangazo ya kibiashara

Sheria hiyo mpya inatarajiwa kupandisha utozwaji kodi kwa wamiliki wa migodi mbalimbali nchini humo baada ya kupitishwa na bunge mwezi Januari.

Wamiliki wa migodi hata hivyo, wamekuwa wakitoa wito kwa rais Kabila kutotia saini sheria hiyo kwa sababu itasababisha wawezekani kuondoka na kutokuja nchini DRC kuwekeza katika sekta hiyo.

Waziri anayehusika na masuala ya madini Martin Kabwelulu amethibitisha kufanyika kwa mkutano huo kupitia ujumbe wake mfupi kwa Shirika la Habari la Reuters lakini hakueleza kwa kina kuhusu mazungumzo hayo.

DRC ni nchi tajiri duniani kwa madini ya Cobalt na mwaka 2017, ilichimba tani 73,940 ya madini ya Cobalt.

Licha ya utajiri huu, raia wa nchi hiyo wameendelea kuishi kwa umasikini mkubwa hasa wakaazi wa Mashariki mwa nchi hiyo.

Machafuko Mashariki mwa nchi hiyo kwa kiasi kikubwa yamesababishwa na utajiri huo wa madini.

Wataalamu wa maswala ya uchumi na mawakili wa shirikisho lijulikanalo kama Makutano wanaitaka serikali kutetea maslahi ya taifa, katika majadiliano hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.