Pata taarifa kuu
LIBYA-ITALIA-WAHAMIAJI-USALAMA

Wahamiaji 90 wamekufa maji katika bahari Mediterranean

Takriban wahamiaji 90 waliripotiwa kufa maji baada ya boti lao kuzama mapema asubuhi leo Ijumaa akatika pwani ya Libya, Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM) limeripoti.

Wahamiaji waliokolewa nakikosi cha ulinzi wa bahari cha Libya wawasili katika bandari ya Tripoli mnamo Novemba 6, 2017.
Wahamiaji waliokolewa nakikosi cha ulinzi wa bahari cha Libya wawasili katika bandari ya Tripoli mnamo Novemba 6, 2017. REUTERS/Ahmed Jadallah
Matangazo ya kibiashara

Wengi wa wahamiaji hawa ni kutoka Pakistan, manusura walisema.

Mpaka sasa watu watatu ndi wanaaminika kwamba walinusurika na tukio hilo, na miili kumi imeokolewa na kuwekwa kando ya bahari IOM imesema.

"Wametoa idadi ya watu 90 waliokufa maji baada ya boti lao kuzama, lakini tunapaswa kuangalia idadi halisi ya watu waliokufa maji wakati wa tukio hilo," amesema msemaji wa IOM Olivia Headon, akizungumza akiwa Tunis, mji mkuu wa Tunisia, kwa mujibu wa shirika la habari la AFP.

Wahamiaji haramu zaidi ya 600,000 walifanya safari hatari kati ya Libya na Italia katika miaka minne iliyopita. Kwa mwaka huo, wahamiaji 6,624 waliingia Ulaya kupitia bahari Mediterranean, kwa mujibu wa IOM, na wengine 246 walikufa maji wakijaribu kuvuka bahari Mediterranean.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.