Pata taarifa kuu
LIBERIA-SIASA

Weah: Waliberia watashuhudia mabadiliko makubwa

Raia wa Liberia, wameendelea kusherehekea kuapishwa kwa rais wao mpya George Weah. George Weah, mwanasoka wa zamani wa klabu za Ac Milan, Monaco, PSG, Manchester City na mshindi wa Tuzo ya Ballon d’Or 1995, atakua na kazi kubwa ya kuimarisha uchumi katika kipindi cha miaka 6.

George Weah na mkewe Clar, Monrovia tarehe 22 Januari 2018.
George Weah na mkewe Clar, Monrovia tarehe 22 Januari 2018. REUTERS/Thierry Gouegnon
Matangazo ya kibiashara

Mchezaji huyo wa zamani wa mchezo wa soka, aliapishwa jana jijini Monrovia katika sherehe zilizoshuhudiwa na maelfu ya wananchi, marais kadhaa kutoka barani Afrika na wachezaji wa zamani wa mchezo wa soka.

Rais Weah, ameahidi kupambana na ufisadi, kuheshimu haki za kibinadamu na demokrasia, kuunda nafasi za kazi kwa vijana miongoni mwa masuala mengine.

Wiki tatu zilizopia Rais mteule wa Liberia George Weah alitangaza malengo muhimu kwa kipindi chake cha miaka sita, akiahidi kufanya mageuzi makubwa kwa nchi yake hasa katika sekta ya kilimo na ukarabati wa miundombinu.

Katika mahojiano yake ya kwanza tangu kupata ushindi wa zaidi ya 60% ya kura katika duru ya pili ya uchaguzi wa urais, nyota wa zamani wa soka, mwenye umri wa miaka 51, alieleza mipango yake akiweka mbele kilimo.

George Weah, ambaye amemrithi Ellen Johnson Sirleaf, mshinda wa tuzo ya amani ya Nobel, madarakani tangu Januari 2006, alitangaza kuwa yuko tayari kuwafungulia milango wawekezaji wa kigeni na kukabiliana na janga la rushwa linalodidimiza nchi ya Liberia.

Zaidi ya asilimia 60 ya Waiberia hufanya kazi katika sekta ya kilimo, ambako raia wa kigeni waliwekeza katika mashamba ya mafuta ya mitende. Lakini kilimo kinaendelea kushuka kwa sababu ya uzalishaji mdogo, na kupelekea nchi kuagiza nje zaidi ya asilimia 80 ya vyakula vinavyohitajika.

Rais mteule, mzaliwa wa kitongoji cha Clara Town, Monrovia, pia aliahidi kuboresha miundombinu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.