Pata taarifa kuu
CAR-USALAMA

Maelfu ya watu wakimbia mapigano kati ya makundi hasimu ya waasi

Mamia ya watu Kaskazini Magharibi mwa Jamhuri ya Afrika ya Kati, wamekimbia makwao baada ya kutokea kwa mapigano kati ya makundi ya waasi.

Askari wa kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (Minusca) kinaendelea kutoa ulinzi kwa raia. Minusca
Askari wa kikosi cha Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati (Minusca) kinaendelea kutoa ulinzi kwa raia. Minusca MARCO LONGARI / AFP
Matangazo ya kibiashara

Madaktari wasiokuwa na mipaka MSF, wamesema mapigano yalizuka Jumapili iliyopita katika mji wa Paoua, eneo ambalo pia maelfu ya watu waliyakimbia makwao mwezi Novemba mwaka uliopita.

Ripoti zinasema kuwa, baadhi ya watu walishambuliwa kwa mapanga na kujeruhiwa kwa risasi baada ya kulengwa na waasi hao.

Waasi wanaojiita Liberation of the Central African Republic na Revolution and Justice (RJ) wamekuwa wakipambana katika mji huo tangu mwezi Novemba na kuzua wasiwasi.

Takwimu za Umoja wa Mataifa na Shirika la Msalaba mwekundu, zinaonesha kuwa kati ya watu 15,000 hadi 17,000 wakiyakimbia makwao kutoka mji huo wa Paoua kuanzia mwezi Desemba mwaka uliopita.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.