Pata taarifa kuu
DRC-SIASA

Wanaharakati watatu wa kisiasa waachiliwa huru nchini DRC

Wanaharakati watatu wa kisiasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo waliokuwa wanazuiliwa kwa miezi mitano wameachiliwa huru.

Waandamanaji wa upinzani nchini DRC wakiwa kwenye barabara za jiji la Kinshasa.
Waandamanaji wa upinzani nchini DRC wakiwa kwenye barabara za jiji la Kinshasa. DR
Matangazo ya kibiashara

Wanaharakati hao Jean Mulenda, Jean-Pierre Tshisitshabu na Patrick Mbuya, walikamatwa mjini Lubumbashi baada ya kupanga maandamano ya kumshinikiza rais Joseph Kabila kuondoka madarakani lakini pia kuitaka Tume ya Uchaguzi kutangaza tarehe ya Uchaguzi Mkuu.

Shirika la kutetea haki za binadamu la Justicia ASBL lenye makao yake mjini Lubumbashi, limethibitisha kuachiwa huru kwa wanaharakati hao baada ya kutumikia kifungo cha miezi mitano jela.

Hawa ni miongoni mwa mamia ya wanaharakati ambao wametiwa mbaroni na maafisa wa usalama katika harakati za kisiasa nchini humo. Wengi bado wanashikiliwa maeneo mbalimbali nchini humo.

Tume ya Uchaguzi CENI tayari imetangaza ratiba ya Uchaguzi Mkuu, ambao sasa utafanyika tarehe 23 mwezi Desemba 2018.

Rais Joseph Kabila, ambaye muhula wake wa kukaa madarakani unafika mwisho, hivi karibuni alitia saini sheria mpya ya Uchaguzi, ambayo inapingwa na wanasiasa wa upinzani.

Upinzani unasema kuwa, sheria hii inalenga kumwekea mazingira rais Kabila kuwania tena urais kwa muhula wa tatu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.