Pata taarifa kuu
MISRI-USALAMA

Shambulio dhidi ya kanisa laua watu zaidi ya tisa kusini mwa Cairo, Misri

Watu wasiopungua kumi wameuawa katika shambulio dhidi ya kanisa kusini mwa Cairo, nchini Misri. Shambulio hilo limetokea leo Ijumaa (Desemba 29). Makanisa nchini Misri yamekua yakilengwa na mashambulizi ya waislamu wenye msimamo mkali.

Shambulizi lililenga kanisa la Mar Mina katika kusini mwa Cairo.
Shambulizi lililenga kanisa la Mar Mina katika kusini mwa Cairo. REUTERS/Amr Abdallah Dalsh
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa ripoti za awali, mshambuliaji alijaribu kuingia katika kanisa la Mar Mina katika eneo la Helwan, kusini mwa mji wa Cairo.

Polisi waliokua wakitoa ulinzi mbele ya kanisa walimshukia na kuweza kumzuia. Kisha akawafyatua risasi polisi ambao walijibu. Polisi kadhaa wameuawa na wengine wamejeruhiwa, huku mshambuliaji akiuawa kwa kupigwa risasi, kwa mujibu wa chanzo cha usalama. Ripoti ya awali ilikua ilibaini vifo vya watu watanu, lakini ilirekebishwa upya na Wizara ya Afya ya Misri ambayo imesema watu wasiopungua 10 wameuawa katika shambulio hilo.

Shambulizi hili linathibitishwa kuwa waumini wa Kanisa la Coptic bado wanaendelea kulengwa na Waislamu wenye msimamo mkali. Makanisa matatu yamelengwa tangu mwezi Desemba 2016. Wakristo 100 waliuawa katika mashambulizi hayo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.