Pata taarifa kuu
DRC-MONUSCO-TANZANIA

Wanajeshi 15 wa Umoja wa mataifa wauawa nchini DRC

Umoja wa mataifa umethibitisha kuwa askari 15 wa kulinda amani wameuawa eneo katika linaloshuhudia utovu wa usalama mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo ambapo 14 kati yao ni wa Tanzania.

Baadhi ya wanajeshi wa Monusco wakiwa jimboni Kivu Kaskazini nchini DRC
Baadhi ya wanajeshi wa Monusco wakiwa jimboni Kivu Kaskazini nchini DRC REUTERS/Kenny Katombe/File Photo
Matangazo ya kibiashara

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ameshutumu vikali shambulio hilo na kuliita ni uhalifu wa kivita.

Aidha Guterres Ameitaka DR Congo kufanya uchunguzi kuhusu shambulio hilo na kusema kwamba waliohusika wanapaswa kuwajibishwa kwa mujibu wa sheria.

Shambulio hilo lilitekelezwa Alhamisi jioni kwenye kambi ya jeshi ya Semuliki eneo la Beni katika mkoa wa Kivu Kaskazini.

Eneo la mashariki mwa DRC limekuwa likishuhudia ukosefu wa usalama kufuatia makabiliano kati ya vikosi vya serikali na makundi ya wanamgambo lakini pia mapigano ya kikabila ambayo yameonezeka katika siku za hivi karibuni.

Tukio la kuuawa kwa wanajeshi wa Umoja wa mataifa nchini DRC linakuja wakati leo Tanzania bara iliyokuwa Tanganyika ikiadhimisha miaka 56 ya uhuru.

 

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.