Pata taarifa kuu
BURUNDI-TANZANIA

Cenared wataka shinikizo la awamu nyingine ya mazungumzo ya amani Burundi

Upinzani wa Burundi unaoishi nje ya taifa hilo umeitaka jumuiya ya kikanda kutoa shinikizo zaidi katika kufanikisha awamu nyingine mpya ya Mazungumzo Ya amani, kauli ambayo inakuja baada ya kumalizika kwa awamu ya nne ya mazungumzo ya Arusha kaskazini mwa Tanzania.

Benjamin Mkapa,Muwezeshaji wa mazungumzo ya mzozo kuhusu Burundi
Benjamin Mkapa,Muwezeshaji wa mazungumzo ya mzozo kuhusu Burundi EBRAHIM HAMID / AFP
Matangazo ya kibiashara

Aidha Upinzani unaoishi nje ya Burundi, Cenared kwanza umepinga jaribio lolote la kufanyiwa marekebisho ya katiba ya nchi hiyo pia umeelezea kuwa kuna udhaifu ambao umejitokeza upande wa usuluhishi wa mazungumzo ya amani.

mazungumzo hayo ya awamu ya nne yalimalizika hapo jana chini ya mwezeshaji, rais mstaafu wa Tanznia Benjamin Mkapa, ambaye alionyesha kuwa amesikitishwa na mwenendo wa washiriki katika mazungumzo ambao waliendelea kushikilia misimamo yao, na kushindwa kufikia mwafaka kwa manufaa ya wananchi wa Burundi.

Ntahiraja Therence ni msaidizi wa karibu wake waziri wa mambo ya ndani aliyeongoza wajumbe wa serikali, amesema wameridhika na hatua ambayo wameifikia mpaka sasa.

Mwezeshaji wa mazungumzo haya amekusanya maoni ya pande zote zilizokutana kwa mazungumzo ambayo atamkabidhi msuluhishi mkuu rais Yoweri Museveni wa Uganda na kwa wakuu wa nchi za afrika ya mashariki kwa hatua zaidi, hadi sasa hakuna tangazo lolote lililotolewa kuhusu lini pande zote hizi zitakutana kwa mara nyingine tena kwa mazungumzo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.