Pata taarifa kuu
LIBYA-SAHEL-UFARANSA-USALAMA

Wahamiaji wa Kiafrika kutoka Libya kurejeshwa nyumbani

Mkutano wa kwanza wa kuandaa kuwarudisha nyumbani wahamiaji kutoka Libya unatazamiwa kufanyika leo Jumatatu Desemba 4. Umoja wa Afrika unakutana na washirika wake, EU, UNHCR na Shirikisho la Kimataifa la linaloshughulikia masuala ya wahamiaji (IOM), mjini Addis Ababa, nchini Ethiopia.

Zaidi ya Wahamiaji mia moja wa Cote d'Ivoire walirejeshwa nyumbani kutoka Libya mnamo tarehe 20 Novemba 2017.
Zaidi ya Wahamiaji mia moja wa Cote d'Ivoire walirejeshwa nyumbani kutoka Libya mnamo tarehe 20 Novemba 2017. REUTERS/Luc Gnago
Matangazo ya kibiashara

Taasisi hizo zinakutana kujadili namna ya kuwarejesha nyumbani wahamiaji wanaoendelea kukabiliwa na hali nzito nchini Libya. Mkutano unafuatia video iliorushwa na kituo cha televisheni cha CNN kuhusu kuuzwa kwa wahamiaji kama watumwa, hali ambayo ilisababisha mgawanyiko wa kisiasa na kidiplomasia kati ya baadhi ya nchi za Afrika na Libya.

Umoja wa Afrika, kama taasisi zingine, tangu wakati huo unaonyesha nia ya kuhamasisha ili kusaidia wahamiaji wanaoendelea kukabiliwa na hali nzito nchini Libya.

Katika mkutano wa Umoja wa Afrika Umoja wa Ulaya uliotamatika mwishoni mwa juma lililopita jijini Abidjan nchini Cote d’Ivoire swala kuhusu namna ya kuwarejesha kwa haraka wahamiaji waliokwama nchini Libya katika mazingira hatarishi, lilijadiliwa kwa kina bila hata hivyo kupatiwa jawabu.

Baada ya mkutano huo wa Abidjan swala hili linatarajiwa kujadiliwa pia hii leo kwenye mako makuu ya Umoja wa Afrika jijini Addis Abeba nchini Ethiopia, wawakilishi wa Umoja wa Ulaya pamoja na washauri wa Umoja wa mataifa watahudhuria katika mkutano huo.

Hata hivyo hali inaelezwa kuwa mbaya zaidi nchini Libya, kwa mujibu wa Amiral el Fdili, afisaa wa maswala ya jamii.

 

Swala la uundwaji wa kikosi cha pamoja cha kukabiliana swala zima la wahamiaji limeendelea kuzua mkaganyiko huku baadhi wakilipokea ndivyo sivyo.

Hata hivyo, msemaji wa serikali ya Ufaransa Benjamin Griveaux amesema Ufaransa haitoingilia kijeshi bali watakuwepo kwa ajili ya kutoa Mafunzo.

“Ufaransa haitoingiliaji kijeshi, inabidi uwepo wa kikosi cha mseto kutoka Afrika ambacho kinaweza kuingilia, Ufaransa na Umoja wa Ulaya wanawza kiuwepo kwa ajili ya kutoa mafunzo”, Benjamin Griveaux.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.