Pata taarifa kuu
UFARANSA-MISRI-HRW-HAKI

HRW yaomba Ufaransa kuachana na sera ya ustahimilivu kwa Misri

Shirika la kimataifa la Haki za Binadamu la Human Right Watch limemtolea wito Rais Emmanuel Macron kukomesha "sera ya ustahimilivu" ya Ufaransa kwa "serikali ya kiimla" ya Rais wa Misri Abdel Fattah al Sissi.

Aliye kuwa rais wa Ufaransa François Hollande akiongozana na Abdel Fatah al-Sisi katika ikulu ya Elysée Novemba 26, 2014.
Aliye kuwa rais wa Ufaransa François Hollande akiongozana na Abdel Fatah al-Sisi katika ikulu ya Elysée Novemba 26, 2014. Reuters
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Misri Abdel Fatah Al-Sissi anaanza Jumatatu hii ziara ya siku tatu nchini Ufaransa. Katika taarifa iliyotolewa na Human Right Watch, imeitaka Ufaransa, mwekezaji wa wasita wa kigeni nchini Misri na mmoja wa wauzaji wake wakuu wa silaha chini ya utawala wa François Hollande, kutoa msaada wake kwa masharti ya "maboresho muhimu" kwa haki za binadamu.

Kwa mujibu wa Human Right Watch, Abdel Fattah Al-Sisi aliongoza, tangu kuchukua hatamu ya uongozi wa nchi mwaka 2014, "mgogoro mkubwa wa haki za binadamu ulioikumba nchi ya Misri kwa miongo kadhaa", huku akiwaweka nguvuni maelfu ya wapinzani.

Human Right Watch pia imeshtumu vikosi vya usalama vya Misri kuwafanyia mateso wafuasi wa upinzani.

Ikulu ya Elysée ilisema wiki iliyopita kuwa suala la haki za binadamu litajadiliwa wakati wa ziara ya rais wa Misri, ambaye pia atakutana na wakuu wa makampuni ya Kifaransa.

Bénédicte Jeannerod, mkuu wa Human Right Watch kwa Ufaransa, amesema katika taarifa yake kwamba Emmanuel Macron "hatakiwi kufuata sera ya kuvumiliana ya Ufaransa na serikali ya Al-Sissi".

"Kudai kuwa suala la haki za binadamu litajadiliwa katika mazungumzo huku kukionekana kuwa hakuana kinachochukuliwa kama hatua itakuwa kama kuweka kukanyaga madai na mateso yanayowakabili wananchi wa Misri," Bénédicte Jeannerod ameongeza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.