Pata taarifa kuu
NIGERIA-BOKO HARAM-USALAMA

Boko Haram yawau watu 5 Nigeria

Watu watano wameuawa baada ya kutokea kwa shambulizi la kujitoka mhanga Kaskazini Mashariki mwa Nigeria. Hali ya usalama inaendelea kutisha katika nchi hiyo.

Askari wa Nigeria wakipiga doria katika wilaya  ya Panshekara, kaskazini mwa mji wa Kano.
Askari wa Nigeria wakipiga doria katika wilaya ya Panshekara, kaskazini mwa mji wa Kano. REUTERS/Radu Sigheti
Matangazo ya kibiashara

Kundi la Boko Haram lilitekeleza shambulizi hilo baada ya kuvamia kijiji kimoja siku ya Alhamisi jioni Kusini mwa mji wa Maiduguri.

Mashambulizi kama haya yameendelea kuzua hali ya wasiwasi kwa raia wa Kaskazini mwa nchi hiyo.

Boko Haram imewaua maelfu ya raia na wengine wengi kuwashikilia kama mateka, huku jumuiya ya kimataifa ikiendelea kulaani vitendo vinavyoendeshwa na kundi hili katika baadhi ya nchi za Afrika ya Magharibi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.