Pata taarifa kuu
CAMEROON-VYOMBO VYA HABARI

Uhuru wa vyombo vya habari: Cameroon yajibu tuhuma dhidi yake

Waziri wa Mawasiliano na msemaji wa serikali ya Cameroon amejibu kuhusu ripoti ya shirika linalotetea Waandishi wa Habari (CPJ) juu ya uhuru wa vyombo vya habari nchini humo.

Issa Tchiroma Bakary, Waziri wa Mawasiliano wa Cameroon.
Issa Tchiroma Bakary, Waziri wa Mawasiliano wa Cameroon. AFP/Pacome
Matangazo ya kibiashara

Issa Tchiroma-Bakary amefutilia mbali mashtaka dhidi ya serikali yake kuwa inaminya uhuru wa vyombo vya habari, huku akihakikisha kuwa nchi yake inaheshimu uhuru wa vyombo vya habari, lakini amekumbusha kwamba Cameroon iko katika vita.

Kauli hii ya serikali inakuja wakati ambapo siku ya Jumatano Septemba 20, rais Paul Biya ambaye anahudhuria Mkutano Mkuu wa Umoja w Mataifa mjini New York.

Shirika linalotetea Waandishi wa Habari (CPJ) lilitoa ripoti hiyo siku ya Jumatano likiishtumu serikali ya Cameroon kuminya uhuru wa vyombo vya habari na kuwafunga bila hatia waandishi wa habari.

"Tuko katika hali ya vita, na nchi zote duniani ambazo ziko katika hali ya vita zina sheria ya kupambana na ugaidi. Katika hili, Cameroon inahusika na ni nchi huru. Ufaransa, kuna sheria za kupambana na ugaidi, nchini Marekani kuna sheria za kupambana na ugaidi, " amesema Issa Tchiroma-Bakary

Ripoti hii inaonyesha tena jinsi sheria ya kupambana na ugaidi ya mwaka 2014 inavyotumiwa kuminya vyombo vya habari au upinzani. Katika suala hili, kesi ya mwandishi wa Idhaa ya Hausa ya RFI, Ahmed Abba, anayezuiliwa jela miaka miwili sasa, ni ushahidi tosha, amesema Robert Mahoney, naibu mkurugenzi wa CPJ.

"Alishtakiwa kwa kukiuka sheria ya kupambana na ugaidi nchini Cameroon na kwa upande wtu hilo ndio shida. Kwa sababu ni sheria ya kupambana na ugaidi ambayo hutumiwa kuminya upinzani nchini Cameroon. Na waandishi wote wa habari wa Cameroon wanaathirika na sheria hiyo. Tumehojiana na waandishi wengi kwa kuandika ripoti hii na wote walituambia kwamba wanaogopa hatari ya kukamatwa au kufungwa kwa magazeti yao na kwamba kuna hali ya wasiwasi nchini humo, "Bw Mahoney amesema.

Waziri wa a Mawasiliano na msemaji wa serikali Issa Tchiroma-Bakary amekanusha mashtaka hayo na kudai kuwa uhuru wa vyombo vya habari unaheshimishwa nchini humo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.