Pata taarifa kuu
CAR-USALAMA

Rais Touadera amtimua waziri wake wa Ulinzi

Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Faustin-Archange Touadera ametangaza kumfuta kazi waziri wake wa ulinzi Joseph Yakete. 

Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Faustin-Archange Touadéra.
Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Faustin-Archange Touadéra. REUTERS/Siegfried Modola/Files
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo taarifa iliyotolewa na ikulu ya Bangui haikusema ikiwa kufutwa kazi kwa Yakete kumetokana na kuendelea kudorora kwa hali ya usalama nchini humo inayochangiwa na vurugu za kikabila na kidini.

Katika tathmini ya hivi karibuni umoja wa Mataifa umeripoti kuwa watu 25 wameuawa ndani ya mwezi huu na wengine maelfu wakilazimika kukimbia makazi yao kwenye maeneo mbalimbali ya nchi.

Hali ya usalama imeendelea kudorora nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Machafuko nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati yamesababisha maelfu ya raia kupoteza maisha na maelfu wengine kukimbilia nchi jirani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.