Pata taarifa kuu
ZIMBABWE-AFRIKA KUSINI-GRACE

Mke wa rais Mugabe kufunguliwa mashitaka Afrika Kusini

Grace Mugabe, mke wa rais wa Zimbabwe Robert Mugabe atafunguliwa mashtaka nchini Afrika Kusini kwa kumdhalalisha mwanamke mmoja jijini Johannesburg.

Mke wa rais wa Zimbabwe, Grace Mugabe.
Mke wa rais wa Zimbabwe, Grace Mugabe. Zanu-PF/handout
Matangazo ya kibiashara

Bi.Mugabe mwenye umri wa miaka 52, anatuhumiwa kuwa alitumia kifaa cha umeme kumpiga na kumuumiza mwanamke huyo Gabriella Engels, mwenye umri wa miaka 20 na kumjeruhi wiki iliyopita.

Mwanamke huyo wa miaka 20 amemshutumu Bi Mugabe wa kumpiga kichwani kwa kifaa cha umeme akiwa hotelini.

Polisi nchini Afrika Kusini walithibitisha kuwa mwanamke huyo alikuwa ameandikisha kesi ya kushambuliwa kwa minajili ya kumsababishia madhara makubwa ya mwili.

Shambulizi hilo linaripotiwa kufanyika siku ya Jumapili jioni.

Bi Mugabe alikuwa nchini Afrika Kusini kutibiwa jeraha alilopata kufuatia ajali ya barabarani mwezi uliopita

Hali hii ilihatarisha uhusiano wa kidiplamasia kati ya nchi hizo jirani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.