Pata taarifa kuu
SIERRA LEONE-USALAMA

Mamia ya watu wapoteza maisha katika maporomoko ya ardhi Freetown

Mamia ya watu bila shaka wanaripotiwa kupoteza miasha katika maporomoko makubwa ya ardhi. Kisa kiliyotokea katika moja ya vitongoji vya mji wa Freetownsiku ya Jumatatu asubuhi, Agosti 14.

Mkazi wa wa eneo la Regent, nje ya jiji la Freetown, ambapo mafuriko yamesababisha mamiaya watu kupoteza maisha Jumatatu, August 14.
Mkazi wa wa eneo la Regent, nje ya jiji la Freetown, ambapo mafuriko yamesababisha mamiaya watu kupoteza maisha Jumatatu, August 14. STR / Society 4 climate change communication Sierra Leone / AFP
Matangazo ya kibiashara

Idadi ya muda ya waliopoteza maisha ambayo mpaka sasa imetolewa ni ya watu 312. Maafisa wa huduma za dharura wako katika eneo la tukio na wanajaribu kuokoa waathirika katika mazingira gumu.

Picha ambazo zimekua zikitolewa zinatisha. Maporimoko makubwa ya adhi yameshuhudiwa katika vijiji na maeneo, huku baadhi ya paa za nyumba zikielea hewani. Waahtirika ambao wamenusurika tukio hilo wamejikuta wakizidiwa na kiwango cha maji ambayo yameendelea kushuhudiwa katika maeneo mbalimbali ya mji mkuu wa Sierra Leone.

Wakazi wa eneo la Regent wakijaribu kukimbia kabla ya maporomoko, Jumatatuhii, Agosti 14, nje kidogo ya mji wa Freetown.
Wakazi wa eneo la Regent wakijaribu kukimbia kabla ya maporomoko, Jumatatuhii, Agosti 14, nje kidogo ya mji wa Freetown. DR / S4CC

Idadi ya watu waliopoteza maisha inaendelea kuongezeka. Idadi ya mwisho ya shirika la msalaba mwekundu nchini Sierra Leone iliyotolewa saa tisa saa za nchini humo ni ya watu 312.

Eneo moja la milima liliporomoka mapema leo Jumatatu kufuatia mvua kubwa, na kusababisha nyumba nyingi kufukiwa kwa mjibu wa maafisa wa usalama.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.