Pata taarifa kuu
UFARANSA-SAHEL-USHIRIKIANO

Waziri wa ulinzi wa Ufaransa azuru baadhi ya nchi za ukanda wa Sahel

Waziri wa ulinzi wa Ufaransa Florence Parly anaendelea na ziara yake katika nchi za ukanda wa Sahel, baada ya Niger.

Waziri wa ulinzi wa Ufaransa, Florence PArly, anaendelea na ziara yake katika nchi za ukanda wa Sahel.
Waziri wa ulinzi wa Ufaransa, Florence PArly, anaendelea na ziara yake katika nchi za ukanda wa Sahel. BENJAMIN CREMEL / AFP
Matangazo ya kibiashara

Katika ziara ambayo Florence Parly anaambatana na mwenziwe wa Ujerumani kuangalia wapi zimefikia shughuli za ujenzi wa kituo cha pamoja cha ulinzi wa nchi tano kukabiliana na ugaidi.

Hapo jana waziri Florence alikkuwa nchini Niger ambapo amekutana na rais Mohamadu Issoufou kwa takriban saa nzima, ambapo mazungumzo yao yametuama kuhusu swala la ulinzi na muendelezo wa harakati za kupambana na Ugaidi.

Akiambatana na mwenziwe wa Ulinzi kutoka Ujerumani, wamezuri pia shughuli za ujenzi wa kambi ya pamoja ya majeshi ya nchi tano ambayo inatarajiwa kuinduliwa mwishoni mwa mwezi Agost mwaka huu.

Waziri huyo wa Ufaransa amesema lengo la ziara yake kama waziri wa ulinzi ni kushuhudia wapi zimefikia shughuli hizo.

Hivi karibuni utafaynika mkutano wa wafadhili jijini Berlin, kwa ajili ya kutoa nafasi kwa wafadhili wengine kujitokeza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.