Pata taarifa kuu
CAMEROON-RFI

Mwanahabari wa RFI Hausa Ahmed Abba atimiza miaka miwili jela

Ni miaka miwili kamili tangu kukamatwa na kuzuiwa kwa Mwanahabari wa RFI Hausa Ahmed Abba, kwa madai ya ugaidi baada ya kupatikana katika eneo la Maroua, Kaskazini mwa nchi ya Cameroon.

Ahmed Abba, Mwanahabari wa RFI Hausa
Ahmed Abba, Mwanahabari wa RFI Hausa www.rfi.fr
Matangazo ya kibiashara

Mwezi Aprili mwaka huu, Mahakama ilimhukumu miaka 10 jela baada ya kumpata na kosa la kushirikiana na magaidi wa Boko Haram, madai ambayo ameendelea kuyakanusha licha ya hukumu hiyo.

Kabla ya kupewa hukumu hii, kulikuwa na wasiwasi wa Abba kupewa adhabu ya kifo kwa mujibu wa sheria za nchi ya Cameroon.

Tayari Mawakili wake wamekata rufaa dhidi ya hukumu hiyo na hadi sasa haijafahamika ni lini kesi ya rufaa itaanza kusikilizwa katika Mahakama ya kijeshi.

Aidha, Mawakili wa Abba wamekuwa wakisema kuwa, kesi dhidi ya Abba haikuwa na uzito wowote kwa sababu viongozi wa mashataka walishindwa kuthibitisha kuwa, mwanahabari huyo wa RFI alikuwa anashirikiana na magaidi hao.

Uongozi wa Radio France International umeendelea kusisitiza kuachiwa huru kwa Abba bila masharti kwa sababu hakufanya kosa lolote.

Kuendelea kuzuiwa kwa Abba, kumeendelea kulaaniwa pia na Shirika la Kimataifa linalotetea maslahi ya wanahabari la RSF ambalo limeendelea kusema kuwa kinachoendelea ni ukiukwaji wa haki za Abba kama mwanahabari.

Mkuu wa Shirika hilo Christophe Deloire, naye pia ameendelea kushinikiza kuachiliwa huru kwa Abba ambaye amesema alikuwa anafanya kazi yake alipokamatwa.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.