Kiongozi wa upinzani nchini Zambia atimiza siku 100 jela
Kiongozi wa upinzani nchini Zambia Hakainde Hichilema ametimiza miaka 100 jela, baada ya kushtakiwa kwa makosa ya uhaini.
Imechapishwa:
Hichilema amesema kwa kipindi chote hicho amekuwa akipitia kipindi kigumu kwa sababu haki zake msingi zinakiukwa na amezuiwa katika mazingira mabaya.
Kupitia ukurasa wake wa Facebook, mwanasiasa huyo ameeleza kuwa pamoja naye, wafungwa wengine pia wanazuiwa katika mazingira yasiyo ya kuridhisha.
“Tunaamini kuwa licha ya makosa ambayo wafungwa hawa wamefanya, na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu kuzuiwa kama mazingira haya mabaya,” ameandika.
“Wengine wetu bado, tunatafuta makosa tuliyofanya,” aliongeza.
Hichilema alikamatwa mapema mwaka huu baada ya msafara wake kuzuia msafara wa rais Edgar Lungu.
Mwanasiasa huyo ameyakanusha madai hayo na kusema ni ya kisiasa yanayotumiwa dhidi yake.