Pata taarifa kuu
BOKO HARAM-CAMEROON

Amnesty International lashtumu jeshi la Cameroon kwa kuwatesa washukiwa wa Boko Haram

Shirika la Kimataifa linalotetea Haki za Binadamu la Amnesty International, linasema makumi ya watu wanahofiwa kupoteza maisha nchini Cameroon mikononi mwa wanajeshi wa serikali.

Baadhi ya wanawake waliotekwa na wapiganaji wa Boko Haram.
Baadhi ya wanawake waliotekwa na wapiganaji wa Boko Haram. Sahara Reporters
Matangazo ya kibiashara

Ripoti ya Shirika hilo inasema kuwa wengi wa watu hao ni washukiwa wa kundi la kigaidi la Boko Haram.

Baada ya kuwahoji watu 101, Amnesty International imesema kuwa watu hao wamesema wanazuiwa katika maeneo ya siri, na kuteswa na kikosi maalum cha jeshi.

Imebainika kuwa washukiwa hao wamekuwa mikononi mwa jeshi la Cameroon tangu mwaka 2013.

Cameroon imeungana na mataifa mengine ya Niger, Nigeria na Chad kupambana na kundi la Boko Haram ambalo limesababisha maelfu ya watu kupoteza maisha na wengine kuyakimbia makwao Kaskazini mwa Nigeria.

Mataifa ya Afrika Magharibi yameendelea kulengwa na kundi la Boko Haram.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.