Pata taarifa kuu
DRC-KATUMBI-HAKI

Kesi ya Moise Katumbi kusikilizwa Lubumbashi

Mahakama mjini Lubumbashi inatarajia kusikiliza hii leo kesi ya rufaa inayomuhusisha gavana wa zamani wa jimbo la Katanga Moise Katumbi na Emmanuel Stoupis ambapo Katumbi alihukumiwa Juni 2016 kifungo cha miaka 3 jela.

Mwanasiasa wa upinzani Moise Katumbi akiasindikizwa na wafuasi wake mahakamani, Lubumbashi, Mei 11, 2016.
Mwanasiasa wa upinzani Moise Katumbi akiasindikizwa na wafuasi wake mahakamani, Lubumbashi, Mei 11, 2016. © REUTERS/Kenny Katombe
Matangazo ya kibiashara

Moise katumbi anatuhumiwa kumpora ardhi Emmanuel Stoupis, kesi ambayo inaagaliwa na wengi kuwa ni kesi ya kisiasa. Kesi hyo ya rifaa itasikilizwa hii leo na mahakama ya Lumbumbashi wakati Moise katumbi mwenye akiwa yupo uhamishoni tangu zaidi ya mwaka mmoja sasa. Hata hivyo hakuna ulazima wa yeye kuwepo mahakamani hapo wakati kesi yake ikisikilizwa.

Juni 22 mwaka jana Mahakama ya amani ya Lubumbashi ilimpa sheria Emmanuel Stoupis aliemshitaki Moise Katumbi kwa kosa la kughushi stakabadhi katika ununuzi wa jengo ambalo lilikuwa urithi wake.

Hata hivyo baada ya hukumu hiyo Jaji mkuu wa mahakama hiyo ya Amani Chantal Ramazani Wazuri aliomba kuondowa saini yake katika hukumu ya kesi hiyo na kwamba alisaini kwa shinikizo ili kumzuia Katumbi kuwania urais.

Chantal Ramazani Wazuri tangu kipindi hicho aliomba hifadhi ya kisiasa nchini Ufaransa.

Maaskofu wa kanisa katoliki nchini DR Congo CENCO wanaiona kesi hii kama usanii mtupu, jambo ambalo serikali ya DRCongo inasema ni kesi ya kawaida inayo wahusisha raia wawili, huku wakili wa Emmanuel akisisitiza kwamba sio kwa vile katumbi ni mwanasiasa ndio itazuia mteja wake kudai haki yake.

Mawakili watetezi wa katumbi wanasema hawana imani na jopo la majaji katika kesi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.