Pata taarifa kuu
AU-USALAMA-SIASA

Mkutano wa AU wamalizika: baadhi waridhika, wengine mashakani

Mkutano wa 29 wa Umoja wa Afrika ulimalizika tangu siku ya Jumanne Juali 4 katika mji mkuu wa Ethiopia Addis Ababa. Baadhi ya wakuu wa nchi waliondoka wakiwa na wasiwasi na wengine wakisema wameridhika.

Ukumbi wa mikutano wa Umoja wa Afrika uliobaitzwa jina la Nelson Mandela katika makao makuu ya Umoja wa Afrika, Addis Ababa.
Ukumbi wa mikutano wa Umoja wa Afrika uliobaitzwa jina la Nelson Mandela katika makao makuu ya Umoja wa Afrika, Addis Ababa. Zacharias ABUBEKER / AFP
Matangazo ya kibiashara

Miongoni mwa wakuu wa nchi walioonyesha wasiwasi wao ni pamoja na rais wa Djibouti Ismail Omar Guelleh. Tangu askari wa Qatar kujiondoa eneo lisilomilikiwa na upande wowote kwenye mpaka na Eritrea, rais wa Djibouti amekua akiomba kuwekwe mipaka kati ya Djibouti na Eritrea. Umoja wa Afrika iko tayari kufanya hivyo na Kamishna wake kwa ajili ya Amani na Usalama, Ismael Chergui, raia wa Algeria, atajaribu kusuluhisha pande hizo mbili, lakini kwa sasa Eritrea inaoneka kuwa haiko tayari kwa mazungumzo.

Tume ya Umoja wa Afrika itatuma timu ya wataalam ili kuchunguza taarifa hizo, Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika ameelezea wanahabari wetu. "Tumeomba Umoja wa Afrika ushughulikie kwa kuweka mipaka kati ya nchi hizi mbili".

Katika mgogoro kuhusu Qatar, "Tumepunguza uhusiano wetu na nchi hiyo, lakini tuna matumaini ya kuona suala hili linapatiwa ufumbuzi wa kudumu kati ya ndugu zetu," alisema rais wa Djibouti.

Azimio dhidi ya vikwazo vitakavyochukuliwa na upande mmoja: DRC yakaribisha

Miongoni mwa wakuu wa nchi walioridhika na mkutano huu wa Umoja wa Afrika, ni pamoja na rais wa DR Congo Joseph Kabila, ambaye alipata uungwaji mkono kutoka kwa marais wenzake wanaolaani vikwanzo vilivyochukuliwa na Ulaya na Marekani dhidi ya DR Congo bila Umoja wa Afrika kushirikishwa. Itafahamika kwamba vikwazo vya Marekani na Umoja wa Ulaya vimechukuliwa dhidi yamaafisa ishirini wa serikali ya Jamhuri ya KIdemokrasia ya Congo.

"Tulizungumzia suala hili hapa na Umoja wa Afrika. Hoja ayetu ilipokelwa vizuri na imekaribishwa na Umoja wa Afrika, " Leonard She Okitundu, Waziri wa mambo ya Nje wa DR Congo aliambia RFI.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.