Pata taarifa kuu
DRC-USALAMA

Serikali ya DRC yakataa wito wa UN kuchunguza machafuko jimboni Kasai

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, imekataa wito wa Umoja wa Mataifa wa kuitaka serikali ya Kinshasa, kuanzisha uchunguzi wa kina na wa Kimataifa kuhusu machafuko yanayoendelea katika majimbo ya Kasai na Kasai ya Kati.

Wanajeshi wa DRC wakiwa katika jimbo la Kasai na Kasai ya Kati
Wanajeshi wa DRC wakiwa katika jimbo la Kasai na Kasai ya Kati Reuters
Matangazo ya kibiashara

Majimbo hayo mawili yameendelea kushuhudia mauaji tangu mwaka 2015 baada ya kuanza kwa makabiliano kati ya wanajeshi wa serikali na waasi wa Kamwina Nsapu.

Umoja wa Mataifa unasema machafuko hayo yamesababisha vifo vya watu zaidi ya 400, huku wengine Milioni 1.3 wakiyakimbia makwao.

Hata hivyo, Mashirika ya kiraia yanaeleza kuwa watu huenda zaidi ya watu 3,000 wameuawa kutokana na mauaji hayo.

Mkuu wa Tume ya Haki za binadamu katika Umoja huo Zeid Ra'ad Al Hussein, amesema ameipa serikali ya Kinshasa siku mbili kuanzisha uchunguzi huo.

Hata hivyo Waziri anayeshughulikia maswala ya Haki nchini humo Marie-Ange Mushobekwa, amesema hakuna anayeweza kulipagia taifa hilo huru, jambo la kufanya.

Wiki hii, Marekani ilitia wito kwa Umoja wa Mataifa kuanza kufanya uchunguzi wa mauaji ya watalaam wake wawili waliouawa katika jimbo hilo mwezi Machi.

Serikali ya DRC tayari, imefungua kesi dhidi ya washukiwa waliokamatwa kuhusiana na kifo cha watalaam hao Michael Sharp na Zaida Catalan.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.