Pata taarifa kuu
LIBYA-WAHAMIAJI-USALAMA

Wahamiaji wakabiliwa na majanga mbalimbali katika pwani ya Libya

Wahamiaji waendelea kukumbwa na majanga mbalimbali tangu saa 24 zilizopita katika pwani ya Libya. Boti kadhaa zimeonekana na abiria wameokolewa na meli za maafisa wa uokoaji.

Wahamiaji wamekwama na wakiwa katika hali ya dhiki kwenye boti katika pwani ya Libya.
Wahamiaji wamekwama na wakiwa katika hali ya dhiki kwenye boti katika pwani ya Libya. © Malta-based NGO Migrant Offshore Aid Station (MOAS)
Matangazo ya kibiashara

Boti nyingi zimekua zikizama na kusababisha maafa makubwa kutokana na kubeba watu kupita kiasi ya uwezo zilizokadiriwa.

Mashirika ya kibinadamu yana jukumu muhimu katika operesheni ya uokoaji tangu siku ya Jumanne kwa karibu watu 2 500. Na siku Jumatano hii, shughuli hii imeendelea.

Majanga kadhaa yamekua yakishuhudiwa katika pwani ya Libya . Kila mtu anaweza kufahamu hilo, kwa sababu waandishi wa habari wengi wanaambatana na maafisa wa uokoaji na wamekua wakitoa taarifa mbalimbali kuhusu hali hiyo inayoendelea kushuhudiwa katika pwani ya Libya kwa sasa. Mapema siku ya Jumatano mchana, operesheni ya uokoaji imekua ikiendelea kwa kuwaokoa abiria 700 waliokua wakisafiri na boti lililotengenezwa kwa mbao wakiwa katika hali ya dhiki.

Shughuli hii inahusisha meli nyingi, ikiwa ni pamoja na, Phoenix ya shirika la kihisani la MOAS, ambayo inasaidizana na meli ynigne za kibiashara, lakini pia kikosi cha wanamaji cha Italia. Kwa sasa, kinachojulikana tu ni kwamba miili kadhaa inaelea kwenye bahari karibu na boti lililozama, ikiwa ni pamoja na miili ya watoto, kwa mujibu wa abiria mmoja anayesafiri katika meli ya shirika la Phoenix.Kikosi cha wanamaji cha Italia kinabaini kwamba tayari kimewaokoa watu 20. Kwa hakika, watu kadhaa wamedondoka ndani ya maji wakati ambapo shughuli za uokoaji zilikua zimeanza, pengine kutokana na mawimbi makubwa.

Watu 1,800 walikua katika hali ya dhiki siku ya Jumanne

Janga hili linakuja siku moja baada ya jinamizi jingine. Tangu siku ya Jumanne, Maafisa wa meli tatu za mashirika yasiyo ya kiserikali walikua wakiwaokoa takriban watu 1,800 waliokua katika hali ya dhidi na manung'uniko ambao walikua wakisafiri na boti zilizokua zimepotea kwenye bahari ya Libya wakati ambapo ghafla boti ndogo za kikosi cha walinzi wa pwani ya Libya walipowasili na kuanza kutumia silaha kwa kuwatia uoga.

Haijulikani aliyekua akilengwa, lakini inasemekana wahamiaji kutokana na uoga baadhi walidondoka ndani ya bahari, lakini waliweza kjunusurika kutokana na mavazi maalumu waliokua wamevaa ambayo walipewa na mashirika yasio ya kiserikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.