Pata taarifa kuu
SOMALIA-USALAMA

Uwanja wa ndege wa Mogadishu washambuliwa

Kwa mujibu wa vyanzo vya usalama kutoka mji mkuu wa Somalia Mogadishu, mabomu kadhaa yamerushwa dhidi ya uwanja wa ndege wa Mogadishu.

Uharibifu mkubwa unaofanywa na makundi yenye silaha nchini somalia.
Uharibifu mkubwa unaofanywa na makundi yenye silaha nchini somalia. REUTERS/Feisal Omar
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa maafisa wa usalama mshambuliaji mmoja aliuwawa, baada ya polisi kukabiliana kundi la watu wenye silaha ambao walikua wakiendesha shambulio katika uwanja wa ngege wa mji mkuu wa Somalia, Mogadishu. Mpaka sasa hakuna kundi ambalo limedai kuendesha shambulio hilo.

Mashahidi wanasema askari wa usalama wa Somalia walipambana kwa risasi, na washambuliaji ambao hawajajulikana ni kutoka kundi gani.

Hayo yakijiri Shirika la Chakula Duniani, WFP, inasema kumetokea mlipuko mita mia moja kutoka msafara wake mjini Mogadishu.

WFP imesema inachunguza kama mlipuko huo ulilengwa dhidi ya msafara wake.

Ni miaka kadhaa sasa Somalia ikiendelea kukumbwa na mashambulizi ya makundi yenye silaha, licha ya Umoja wa Afrika kutuma askari wake ili kusimamia amani nchini humo.

Watu kadhaa wamepoteza maisha katika mashambulizi mbalimbali yanayotekelezwa na makundi mbalimbali ya silaha, hasa kundi la Al Shabab.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.