Marekani yatangaza vikwazo dhidi ya viongozi wa makundi ya waasi wa Seleka na Anti Balaka
Marekani imetangaza vikwazo dhidi ya viongozi wawili wa makundi ya uasi nchini Jamhuri ya Afrika ya kati.
Imechapishwa:
Washington DC inasema wawili hao ni Abdoulaye Hissene anayeongoza kundi la lenye mrengo wa Kiislamu la Seleka na Maxime Mokom kiongozi wa kundi lenye mrengo wa Kikiristo Anti-Balaka.
Marekani inasema viongozi hao wameendelea kusababisha nchi ya Afrika ya Kati kutokuwa na utulivu kutokana na mashambulizi ya mara kwa mara.
Mali zao zimezuiliwa na Marekani lakini haijabainika ikiwa wana mali yoyote nje ya nchi.
Pamoja na hilo, raia wa Marekani wamepigwa marufuku ya kushirikiana na wawili hao kwa lolote.
Mzozo wa Jamhuri ya Afrika ya Kati ulianza mwaka 2012 baada ya waasi wa Seleka kumwondoa madarakani rais wa wakati huo Francois Bozize.
Watu zaidi ya elfu tano wamepoteza maisha na wengine zaidi ya 700,000 kuyakimbia makwao kwa muda miaka minne sasa.