Pata taarifa kuu
DRC-USALAMA

Polisi 40 wauawa Kasai DRC

Kundi la wapiganaji wa Kamwina Nsapu nchini DRC limetekeleza mauaji ya maafisa 40 wa polisi katika shambulizi jimboni kasai,maafisa katika eneo hilo wamearifu.

Baadhi ya wapiganaji wa zamani wa wakiwasili Kananga
Baadhi ya wapiganaji wa zamani wa wakiwasili Kananga RFI/Sonia Rolley
Matangazo ya kibiashara

Shirika la habari la Uingereza BBC Limeripoti kuwa wapiganaji wa kundi la Kamwina Nsapu walishambulia msafara wa maaskari hao.

kiongozi wa Kasai Francois Kalamba ameeleza kuwa askari sita waliachiwa huru lakini wengine walichinjwa.

Machafuko katika jimbo la Kasai yalianza mnamo mwezi August mwaka jana baada ya vikosi vya usalama kumuua kiongozi wa kundi hilo la Kamwina Nsapu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.