Pata taarifa kuu
CAF-SOKA-UCHAGUZi

Rais mpya wa CAF kuchaguliwa Alhamisi hii

Uchaguzi mkuu wa rais wa Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF) unafanyika Alhamisi hii Machi 16 katika makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa, nchini Ethiopia. Issa Hayatou, rais wa shirikisho hilo anayemaliza muda wake anachuana na Ahmad Ahmad, rais wa chama cha Soka nchini Madagascar.

Ahmad Ahmad, rais wa chama cha Soka nchini Madagascar na mgombea urais wa Shirikisho la Soka la Afrika (CAF).
Ahmad Ahmad, rais wa chama cha Soka nchini Madagascar na mgombea urais wa Shirikisho la Soka la Afrika (CAF). RIJASOLO / AFP
Matangazo ya kibiashara

Issa Hayatou kutoka Cameroon, anatetea nafasi yake anayoishikilia toka mwaka 1988.

siku ya Jumatano mshindani wa Issa hayatou, Ahmad Ahmad, alikua akihamasisha na kuwashawishi marais wa vyama vya soka kutoka nchi mbalimbali mjini Addis Ababa kumpigia kura. Bw Ahmad ameendelea kuamini kwamba anaweza kumuangusha Issa Hayatou Cameroon.

Itafahamika kwamba Ahmad Ahmad hakuhudhuria filamu ya miaka 60 ya Shirikisho la Soka barani Afrika (CAF).

Issa Hayatou, raia wa Cameroon, anatetea nafasi yake anayoishikilia toka mwaka 1988.
Issa Hayatou, raia wa Cameroon, anatetea nafasi yake anayoishikilia toka mwaka 1988. GHANAsoccernet

 Duru za kuaminika zinasema kuwa, kumekua kukifanyika mazungumzo ya chini kwa chini kuhusu uchaguzi wa wajumbe wa Kamati ya Utendaji, uchaguzi wa wawakilishi wa Afrika kwenye Baraza la Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) na uchaguzi rais mpya wa CAF.

"Sawa, mambo yanakwenda vizuri, " amesema Ahmad kuhusukuwania kwake, kabla ya kwenda kufanya kukutana na wale wanaomuunga mkono.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.