Pata taarifa kuu
NIGERIA-BOKO HARAM-USALAMA

Uhaba wa maji waripotiwa kaskazini-mashariki mwa Nigeria

Maelfu ya watu ambao walikimbia mapigano kati ya Boko Haram na jeshi la serikali kaskazini-mashariki Nigeria wanakabiliwa na uhaba wa maji, huku ukosefu wa chakula na mdoror wa usalama vikiendelea kushuhudiwa katika eneo hilo.

Mwanamke huyu katika kambi ya wakimbizi wa ndani akitafuta maji.
Mwanamke huyu katika kambi ya wakimbizi wa ndani akitafuta maji. Getty Images
Matangazo ya kibiashara

Karibu pampu zote zinazotumiwa kwa kutoa maji katika kambi ya wakimbizi wa ndani ya Muna, katika eneo la Maiduguri, mji mkuu wa jimbo la Borno, hazifanyi kazi, kwa mujibu wa mratibu wa suala la kibinadamu wa kambi hiyo, Tijjani Lumani.

Maji yanayotolewa katika visima kwa mfumo wa pampu za nishati ya jua, hutumika kwa ajili ya kupikia, lakini pia kwa ajili ya kuoga.

Hali hii inawatia wasiwasi maafisa wa mashirika ya misaada ya kibinadamu, ambao wana hofu ya kuenea kwa magonjwa yanayotokana na usafi mdogo.

Gavana wa jimbo la Borno, Kashim Shettima, amethibitisha kuwa kuna "tatizo la kusafirisha maji" katika kambi ya wakimbizi wa ndani ya Muna, lakini kwamba wafanyakazi wanajikita kwa kutata ufumbuzi wa tatizo hilo.

Vita kati ya wapiganaji wa kundi la Boko Haram na jeshi vimesababisha vifo vya zaidi ya watu 20,000 tangu mwaka 2009 na watu milioni 2.6 wameyakimbia makazi yao. Karibu milioni kati yao wamekimbilia katika mji wa Maiduguri.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.