Pata taarifa kuu
DRC-UNSC-MAUAJI

Serikali ya DRC yafutilia mbali ripoti ya Umoja wa Mataifa

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imejibu baada ya ripoti ya Umoja wa Mataifa kutuhumu polisi kuwaua waandamanji kwa makusudi mjini Kinshasa.

Waziri wa habari na msemaji wa Serikali ya DRC, Lambert Mende akifutilia mbali ripoti ya Umoja wa Mataifa inayoituhumu polisi kuwaua waandamanji kwa makusudi mjini Kinshasa
Waziri wa habari na msemaji wa Serikali ya DRC, Lambert Mende akifutilia mbali ripoti ya Umoja wa Mataifa inayoituhumu polisi kuwaua waandamanji kwa makusudi mjini Kinshasa Reuters
Matangazo ya kibiashara

Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imefutilia mbali ripoti hiyo na kusema kwa ni mambo yaliyopangwa kwa kuchafua viongozi wa DR Congo

Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa, watu wasiopungua 40 waliuawa katika matukio haya wakati ambapo serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imebaini kwamba watu 31 pekee ndio waliouawa.

"Serikali inabaini kwamba hakuna ukweli wowote kattika ripoti hiyo, ni mambo yaliyotengenezwa kwa kuweza kuchafua viongozi wa DR Congo," amesema Lambert Mende, msemaji wa serikali ya DR Congo.

Katika maoni yake, "lengo la ripoti hiyo ilikua kudhoofisha mahakama, taasisi za kisiasa na kiusalama vya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na si kwa waathirika kutendewa haki."

Ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa, iliyotolewa Jumanne, inaeleza ukiukwaji unaodaiwa kufanywa na vikosi vya usalama kwa waandamanji walioandamana dhidi ya Kabila mwezi Desemba 2016.

Katika ripoti ya Umoja wa Mataifa, imeelezwa kuwa baadhi ya waandamanaji waliuawa kwa kupigwa risasi na jeshi la polisi.

Upinzani unapinga Joseph Kabila kuendelea kusalia madarakani wakati ambapo muhula wake wa pili ungelimalizika tarehe 19 Desemba 2016.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.