Pata taarifa kuu
SOMALIA-AL SHABAB-USALAMA

Zaidi ya watu 30 wauawa katika mlipuko Mogadishu

Zaidi ya watu 30 wameuawa na wengine 50 kujeruhiwa katika mlipuko wa bomu lililotegwa ndani ya gari katika mtaa wa Madina, mjini Mogadishu nchini Somalia.

Nchi ya somalia imeendelea kukumbwa na mashambulizi ya kujitoa mhanga na yale yanayoendeshwa kwa kutumia magari yaliyotegwa mabomu.
Nchi ya somalia imeendelea kukumbwa na mashambulizi ya kujitoa mhanga na yale yanayoendeshwa kwa kutumia magari yaliyotegwa mabomu. Mohamed ABDIWAHAB / AFP
Matangazo ya kibiashara

Watu walioendesha shambulio hilo alitumia gari hilo ambalo lilikuwa na vilipuzi na kugharimu maisha ya zaidi ya watu 30 katika mtaa wa Madina kusini mwa Somalia, kwa mujibu wa idara za usalama nchini Somalia.

Shambulio hili ni la kwanza kufanyika katika utawala mpya wa Rais wa Mohamed Abdullahi Farmajo Mohamed ambaye alichukua hatamu ya uongozi hivi karibuni baada ya kuteuliwa na Wabunge na Maseneta wa nchi hiyo.

Jumamosi hii iliyopita afisaa mwandamizi wa kundi la Al Shabab alitangaza kuwa watafanya shambulizi kulenga wafuasi wa rais huyo mpya wakidai kuwa anaendeshwana mataifa ya magharibi.

Hata hivyo mpaka sasa hakuna kundi lolote ambalo limekiri kuhusiana na tukio hilo, hata kama kundi la Al Shabaab linanyooshewa kidole.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.