Pata taarifa kuu
DRC-MAUAJI-USALAMA

Lambert Mende: Video inayoonyesha mauaji ya raia ilitengenezwa

Serikali ya jamhuri ya kidemokrasia ya Congo inasema kuwa vidio iliyoenezwa mwishoni mwa juma lililopita kwenye mitandao ya kijamii ikiwaonyesha askari wa jeshi la serikali ya nchi hiyo FARDC wakiwauwa mamia ya watu wanaosadikiwa kuwa wapiganaji mai mai kusini mwa jimbo la Kasai haina ukweli wowote.

Video inayoonyeshawatu wenye silaha wakiwalia sare ya jeshi la DR Congo wakiwafyatulia risasi raia katika mkoa wa zamani wa Kasai.
Video inayoonyeshawatu wenye silaha wakiwalia sare ya jeshi la DR Congo wakiwafyatulia risasi raia katika mkoa wa zamani wa Kasai. Capture d'écran
Matangazo ya kibiashara

Jeshi hilo limeshutumiwa kwa kuua mamia ya waasi walio tiifu kwa kiongozi wao Kamuina Nsapu aliyeuawa mwezi agosti mwaka huu.

Wiki mbili zilizopita, Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ilishtumu matumizi ya nguvu ya jeshi katika mkoa wa zamani wa Kasai.

Katika viedo hiyo ambayo imezua hali ya sintofahamu nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, wanaonekana watu wenye silaha wakivalia sare ya jeshi la DR Congo wakiwafyatulia risasi raia ambao walikua wakiimba.

Watu walionusurika waliuawa katika maeneo mbalimbali walipokua wakikimbilia.

Awali serikali ya DR Congo na tume ya Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (Monusco) walisema kuwa wanachunguza ili kuthibitisha ukweli kuhusu tukio hilo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.