Pata taarifa kuu
MALI-USALAMA

Mtawa kutoka Colombia atekwa nyara kusini mwa Mali

Mtawa kutoka Colombia ametekwa nyara na watu wenye silaha karibu na mji wa Koutiala katika mkoa Sikasso usiku Jumanne kuamkia Jumatano, Februari 8. Eneo hilo ambalo mpaka sasa linaendelea kukumbwa na vitendo vya ugaidi, linapatikana karibu na mpaka na Burkina Faso, zaidi ya kilomita 300 mashariki mwa mji wa Bamako.

Koutiala ni mji wa mashariki mwa Mali, kilomita chache kutoka mpaka na Burkina Faso.
Koutiala ni mji wa mashariki mwa Mali, kilomita chache kutoka mpaka na Burkina Faso. Google Map
Matangazo ya kibiashara

Kwa mujibu wa Wizara ya Usalama ya Mali, watu wanne, wenye silaha, wenye ngozi nyeusi, "walijitangaza kuwa ni wana jihadi."

"Watu hao walifika mapema katika usiku wa Jumanne katika majengo ya watawa kutoka jamii ya Franciscan Sisters, na kuvunja mlango wa nyumba yao, na kisha waliingia ndani ya majengo na kuondoka na vifaa vyote, ikiwa ni pamoja na kompyuta, " amesema Padre Edmond Dembele, Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu wa Mali. Waliomba kwanza pesa, kisha walichukua funguo za gari la wagonjwa.

Waliondoka na gari hilo, wakiwa pamoja na mtawa huyo kutoka Colombiakidini utaifa Colombia. Kama kilomita tano baada ya kuondoka katika mji huo, watekaji nyarawalitelekeza gari waliko waliiba na kwenda kwenye pikipiki wakielekea katika mpaka na Burkina Faso.

Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu nchini Mali pia amesema kuwa hakuna kundi ambalo limedai kuhusika na utekaji nyara huo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.