Pata taarifa kuu
DRC-MAFURIKO

Wakaazi wa mjini Kinshasa wasalia nyumbani

Maeneo mengi ya mji wa Kinshasa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo yamekumbwa na mafuriko Jumanne hii asubuhi kufuatia kupanda ghafla kwa maji yaliosababishwa na dhoruba kali.

Wakaazi wa mji wa Kinshasa washangazwa Jumanne hii na mafuriko ambayo yalisababisha uharibifu mkubwa.
Wakaazi wa mji wa Kinshasa washangazwa Jumanne hii na mafuriko ambayo yalisababisha uharibifu mkubwa. Getty Images
Matangazo ya kibiashara

Katika eneo la Gombe, kaskazini mwa mji mkuu wa DR Congo, mto wa gombe ulijaa, na kusababisha uharibifu mkubwa.

Hali hiyo imesababisha hofu kuwa huenda kuna watu waliopoteza maisha. Katika eneo la Linguala, mita kadhaa na jengo la Bunge, mamia ya watu wamekua wakijitahidi kuondoa maji ambayo yalivamia makazi yao.

Kwa mujibu wa shahidi aliyohojiwa na BBC Afrique, "kuna magari ambayo yamejaa maji na watu wanakabiliwa na tatizo la kuingia katika eneo lililovamiwa na majii."

Kwa mujibu wa shahidi huyo, "Hali ni ya wasiwasi" wakati ambapo inaelezwa kuwa hasa ni kubwa, licha ya kuwa badi haijabainika kuwa kuna watu waliopoteza maisha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.