Pata taarifa kuu
AU-UONGOZI

Mkutano wa 28 wa AU kuanza Jumatatu

Mkutano wa 28 wa Umoja wa Afrika unaanza Jumatatu Januari 30 ambapo watahudhuria wakuu wa nchi na viongozi wa serikali wa nchi 54 kutoka bara la Afrika. Viongozi hawa wanatazamiwa kujadili maswala muhimu yanayoigawanya jumuiya ya Kiafrika.

Jengo la kisasa ambalo ni makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa ikiwa ni zawadi ya China kwa Afrika. Ujenzi wa jengo hili uligharimu Dola Milioni 200.
Jengo la kisasa ambalo ni makao makuu ya Umoja wa Afrika mjini Addis Ababa ikiwa ni zawadi ya China kwa Afrika. Ujenzi wa jengo hili uligharimu Dola Milioni 200. CTBUH
Matangazo ya kibiashara

Kaulimbiu ya Mkutano huu wa kilele wa 28 wa Umoja wa Afrika (AU), ni "kupata faida kamili ya mgao wa watu kwa kuwekeza katika vijana " utaanza rasmi Jumatatu, Januari 22, katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa.

Baada ya kikao cha kawaida cha Kamati ya wawakilishi wa kudumu (kuanzia tarehehe 22 hadi tarehe 24 Januari) kisha kikao cha Baraza Kuu wakiwepo Mawaziri wa Mambo ya Nje wa nchi wanachama (kuanzi Januari 25 hadi 27), na sasa kikao kinachofuata ni cha Wakuu wa nchi na viongozi wa serikali ambacho kinafunguliwa rasmi Jumatatu, Januari 30.

Kwa mujibu wa vyombo vya habari nchini Ethiopia, serikali imetoa wito kwa jeshi ili kuhakikisha usalama umeimarika katika mji wa Addis Ababa wakati wa mkutano huo.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ethiopia amesema zaidi ya viongozi 4,000 wa ngazi ya juu wanatarajiwa kushiriki katika mkutano huo, ikiwa ni pamoja na Wakuu wa nchi na viongozi wa serikali 37 na Mawaziri wa Mambo ya Nje wasiopungua 49.

Wanatarajiwa pia katika mkutano huo Mfalme wa Morocco Mohammed VI, rais wa Afrika Kusini Jacob Zuma, rais wa Misri Abdel Fatah Al-Sisi, Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari, na wengineo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.