Pata taarifa kuu
RWANDA-UFARANSA

Ufaransa yaidhinisha adhabu ya kifungo cha miaka 25 jela kwa jasusi wa zamani wa Rwanda

Mahakama nchini Ufaransa imeunga mkono adhabu ya kifungo cha hadi miaka 25 jela kwa jasusi wa zamani kutoka Rwanda aliyefungwa baada ya kesi ya kwanza kusikilizwa nchini ufaransa kuhusu mauaji ya kimbari yaliyotokea nchini Rwanda 1994.

Miongoni mwa kumbukumbu ya mabaki ya fuvu la binadamu yaliyotokana na mauaji ya Kimbari nchini Rwanda.
Miongoni mwa kumbukumbu ya mabaki ya fuvu la binadamu yaliyotokana na mauaji ya Kimbari nchini Rwanda. Wikipédia
Matangazo ya kibiashara

Pascal Simbikangwa alipatikana na hatia ya kushiriki mauaji ya kimbari na kula njama za uhalifu dhidi ya ubinadamu katika kesi ya kihistoria kusikilizwa mwaka 2014 ambapo ufaransa ilianza kushughulikia washukiwa wa mauaji waishio nchini humo.

Simbikangwa, mwenye umri wa miaka 56 ambaye zamani alikuwa mlinzi wa raisi,amekuwa akisisitiza kuwa hana hatia alikata rufaa mnamo mwezi Octoba akipinga hukumu dhidi yake.

Mawakili wa Simbikangwa wamelalamikia na kukosoa uamuzi huo.

Shirikisho la kimataifa la watetezi wa haki za binadamu na ambalo lilikuwa miongoni mwa mashirika ya kiraia lilisema hukumu hiyo imepaza sauti za waathirika ambao walikuwa wakisubiri haki kwa zaidi ya miaka 20.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.