Pata taarifa kuu
MOROCCO-AU

Morocco yalaani kile ilichokiita "ujanja" wa Dlamini-Zuma

Wizara ya Mambo ya Nje ya Morocoo inamtuhumu Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika (AU) kuwa pingamizi kwa nchi ya Morocco kurejea katika Umoja wa Afrika.

Mfalme wa Morocco, Mohamed VI, Juni 19, 2015.
Mfalme wa Morocco, Mohamed VI, Juni 19, 2015. REUTERS/Maghreb Agence Press/Pool
Matangazo ya kibiashara

Katika taarifa iliyotolewa Jumatano hii, Morocco inamtuhumu Nkosazana Dlamini-Zuma, raia wa Afrika Kusini, "kujaribu kwa kutumia ujanja mpya wa kuzuia uamuzi wa Morocco wa kurejea kwenye nafasi yake ya asili na halali katika familia yake ya kitaasisi ya Afrika."

Mfalme Mohammed VI wa Morocco kwa miezi kadhaa amekua amekua akifanya jitihada za kuirejesha nchi yake katika Umoja wa Afrika.

Morocco ilijiondoa kutoka Umoja wa Afrika tangu mwaka 1984 kwa kupinga dhidi ya kukubaliwa kwa Jamhuri ya Kiarabu ya Saharaw (Sadr), ambayo inaicukuliakama sehemu ya ardhi yake.

Katika taarifa yake, Wizara ya Mambo ya Nje ya Morocco imemtuhumu Bi Dlamini-Zuma kwa "kuchelewesha bila sababu ya kueleweka, ombi la Morocco kwa wanachama wa Umoja wa Afrika."

Morocco inasema kuwa ilimtuma ombi lake la kutaka kurejea katika Umoja wa Afrika tangu mwezi Septemba 2016 na inasema kuwa Nkosazana Dlamini-Zuma "anaendelea na kasi yake kuzuia" faili ya Morocco, "kwa kuishitukiza utaratibu mpya, usiyokuwa wa kawaida na msingi msingi wowote".

Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika amefutilia mbali barua ya nchi wanachama wa Umoja wa Afrika zinazoiunga mkono, kwa mujibu wa serikali ya Morocco.

Kurudi kwa Morocco katika Umoja wa Afrika lazima kupitishwe kwa kura ya nchi wanachama kwa wingi wa theluthi mbili ya kura.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.