Pata taarifa kuu
ICC-KOFI ANNAN

Kofi Annan: Tunapaswa kuisaidia ICC kuboresha kazi yake, si kujiondoa

Baada ya Burundi, Gambia na Afrika kusini kutangaza kwamba wanajiondoa kutoka Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), nchi hizi kwa ujumla ziliweza kusema kwamba zinapinga utendaji kazi wa Mahakama hii.

Kofi Annan akikosoa uamuzi wa baadhi ya nchi za Farika kujiondoa katika ICC.
Kofi Annan akikosoa uamuzi wa baadhi ya nchi za Farika kujiondoa katika ICC. REUTERS/Denis Balibouse
Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo baadhi ya viongozi mashuhuri walioongozi taasisi za kimataifa kama Kofi Annan, wamepinga kauli hizo na shutma zisizoeleweka wala kuwa na msingi.

"Nchi hizi zimefanya kosa kubwa la kujiondoa kwenye mMahakama ya kimataifa ya Uhalifu (ICC). Inapaswa kujua kwamba watu wa Afrika, hasa waathirika wa uhalifu wa kivita, mauaji ya kimbari na uhalifu dhidi ya ubinadamu, wanaunga mkono ICC, kama serikali nyingi za Afrika zilizo katika mfumo mzuri wa kidemokrasia. Kwa upande wangu mimi, ninaunga mkono ICC kwa sababu uhalifu wa kutisha haupaswi kubaki hivyo bila kuadhibiwa, " Amesema Kofi Annan.

"Mimi ni raia wa Afrika na ni mimi ambaye nilifanya ufunguzi wa mkutano wa Roma mwaka 1998, mkutano ambao ulipelekea kuundwa kwa Mahakama hiyo, na nilikua na furaha kwamba bara langu hasa litaunga mkono Mahakama hiyo. Kumbukumbu ya mauaji ya kimbari bado iko akilini kwa raia wengi wa Afrika. Napenda kuongeza kwamba nchi ya kwanza kutia saini mkataba huo ilikuwa ni nci ya Afrka (Senegal), na kwamba Afrika bado ni kundi kubwa kikanda katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), ikiwa na nchi wanachama 34 kwenye Mkataba wa Roma kwa jumla ya nchi 124, " ameendelea Kofi Annan.

"Sisi pia ndio tulikua mara kwa mara tukikataa rufaa kwenye Mahakama hiyo toka kuanzishwa kwake. Uchunguzi wa kesi nane kati ya tisa unaohusu bara la afrika, uliombwa na nchi za Afrika zenyewe. Mataifa ya Afrika pia yaliunga mkono kupelekwa kwakesi ya Darfur na Libya mbele ya Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), kama ilivyoobwa na Baraza la Usalama. Kesi ya Kenya ni moja peke ambayo ilifunguliwa na ICC, lakini uamuzi huo uliungwa mkono na Wakenya wengi ambao walitaka sheria ifuate mkondo wake baada ya vifo vya ndugu zao 1,300 wakati wa ghasia zilizotokea baada ya uchaguzi wa mwaka 200," amesema Bw Annan.

"Hapana, ICC haingilii masuala ya mahakama za kitaifa. Kama iliingilia katika kesi hizo, ni kwa sababu serikali mbalimbali au mahakama hizo hazikufanya uchunguzi sahihi baada ya uhalifu.ICC inaingilia kati wakati itaonekana kuwa nchi husika haiwezi au haitaki kuwafikisha mahakamani raia wake. Waafrika pia wana haki ya kutendewa haki, hata kama nchi zao hazitofanya hivyo, "ameongeza Bw Annan.

Wadadisi wanasema kuwa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Raia inapaswa kuwa na jukumu kama la ICC.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.