Pata taarifa kuu
MOROCCO-ETHIOPIA

Morocco Mohammed VI atazamiwa kuzuru Ethiopia Ijumaa

Baada ya mkutano wa kimataifa wa mabadiliko ya tabia nchi, Mfalme wa Morocco ataendelea na ziara yake barani Afrika ambapo atazuru nchi ya Ethiopia Ijumaa wiki hii na kisha Madagascar mwishoni mwa mwezi wa Novemba.

Mfalme Mohammed VI atazamiwa kuizuru Ethiopia Ijumaa Novemba 18, 2016.
Mfalme Mohammed VI atazamiwa kuizuru Ethiopia Ijumaa Novemba 18, 2016. AFP PHOTO / HO/ MOROCCAN ROYAL PALACE
Matangazo ya kibiashara

Baada ya mkutano wa kimataifa wa mabadiliko ya tabia nchi (COP22) unaofanyika katika mji wa Marrakech, Mfalme wa Morocco Mohammed VI anatazamiwa kuzuru atafanya ziara nchini Ethiopia Ijumaa na baadaye nchini Madagascar ambapo atahudhuria mkutano wa jumuiya ya nchi zinazozungumza Kifaransa (OIF) utakaofanyika tarehe 26 na 27 Novemba mjini Antananarivo.

Ziara ya nchini Ethiopia ilikua katika pmangilio wa ziara ya Mfalme Mohammed VI wakati wa ziara yake katika ukanda wa Afrika Mashariki hususan nchini Rwanda na Tanzania. Ziara hii iliahirishwa baada ya mazungumzo kwa njia ya simu kati ya Mohammed VI na Waziri Mkuu wa Ethiopia Hailemariam Desalegn.

Ethiopia itakuwa mwenyeji wa mkutano wa Umoja wa Afrika mwezi Januari mwakani. Ombi la Morocco kurejeshwa katika Umoja wa Afrika lilitumwa katika nchi wanachama baada ya Mohammed VI kumuomba Rais wa Chad Idriss Deby Itno tarehe 31 Oktoba, kujadili suala hili na Mwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika, Nkosazana Dlamini Zuma, ambaye alipokea hati hiyo Septemba 22 lakini alikuwa bado hajaiwasilisha kwa wahusika.

Ziara ya Mfalme wa Morocco nchini Ethiopia inalenga kuimarisha uchumi wa nchi hizi mbali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.